• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gutettes aziandikia barua Nchi Wanachama kuhusu maendeleo kwenye mageuzi ya Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2017-05-06 17:01:38

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameziandikia barua Nchi Wanachama akielezea maendleo yaliyopatikana kwenye mipango yake mbalimbali ya mageuzi.

    Msemaji wa Guterres, Stephane Dujarric amesema katibu mkuu huyu anatarajia kuimarisha mageuzi yenye maana ili kufanya Umoja wa Mataifa uendane na dunia ya sasa yenye matatizo na kuhakikisha Umoja huo unaweza kuzihudumia kwa ufanisi nchi zote wanachama katika kufanikisha malengo na kushughulikia changamoto zinazozikabili na fursa kwa pamoja. Pia amesema barua hiyo imeeleza ratiba ya maendeleo juu ya masuala mbalimbali ya mageuzi, ikiwemo usawa wa kijinsia, mageuzi kwenye mfumo wa maendeleo, mageuzi kwenye utaratibu wa amani na usalama, usimamizi wa Umoja wa Mataifa, ofisi mpya ya kupambana na ugaidi, ulinzi wa watu wanaotoa ripoti, kupambana na udhalilishaji wa kijinsia na mengineyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako