• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalam wanasema mwelekeo wa kimataifa unatoa fursa ya kupata maendeleo ya haraka kwa Afrika

    (GMT+08:00) 2017-05-06 17:14:51

    Wataalam wanaohudhuria kongamano la biashara nchini Uganda wamezitaka nchi za Afrika kuchukua fursa ya mwelekeo wa biashara duniani na kutafuta maendeleo ya kasi.

    Mwenyekiti mwenza wa Bodi ya Ushauri wa Kiufundi kwenye Mpango wa Kutengenezwa Afrika Pan Li amesema kwenye mkutano wa biashara kati ya China na Uganda uliofanyika jana mjini Kampala kuwa upatikanaji wa upendeleo wa msamaha wa ushuru kwa bidhaa za Afrika kuingia katika masoko ya Ulaya, Marekani na China na Pendekezo la China la Ukanda Mmoja na Njia Moja vitatoa fursa kubwa kwa bara la Afrika.

    Katika mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika Afrika Kusini mwishoni mwa mwaka 2015, Rais wa China Xi Jinping alitangaza maeneo kumi ya kimkakati ya kuongeza ushirikiano na Afrika katika kipindi cha miaka mitatu kupitia pendekezo la wUkanda Mmoja na Njia Moja.

    Ili kuhakikisha utekelezaji mzuri wa matokeo, China imetangaza kutoa dola bilioni 60 za Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako