• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu kutoka ASEAN na China, Japan na Korea Kusini wajadili uchumi

    (GMT+08:00) 2017-05-06 17:51:33

    Mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini Mashariki ASEAN, pamoja na China, Japan na Korea Kusini wamekutana mjini Yokohama, Japan, wakijadili uchumi wa jumla wa dunia na wa kikanda na ushirikiano wa kifedha kati ya nchi hizo 13 .

    Mkutano huo umesema uchumi wa dunia una mweleko mzuri, na uchumi unaongezeka kwa kasi katika maeneo nchi hizo 13, lakini hatari bado zipo kutokana na kutokea tena kwa vitendo vya kujilinda kibiashara na kubana hali ya uchumi. Nchi hizo zimeahidi kusukuma mbele ongezeko endelevu, lenye uwiano na jumuishi kwa kutumia sera zote zinazohitajika zikiwemo zile za kifedha na mageuzi ya kimuundo. Zimesisitiza kuunga mkono mfumo wa wazi wa biashara na uwekezaji kati ya pande nyingi kwenye msingi wa kanuni husika. Pia zimesema zitaendelea kuimarisha uchunguzi kuhusu mzunguko wa mitaji ili kukabiliana na hatari zitakazoweza kutokea katika maeneo ya nchi hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako