• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Magufuli atuma ujumbe wa rambirambi kutokana na ajali ya basi iliyosababisha vifo vya wanafunzi

    (GMT+08:00) 2017-05-07 16:58:39

    Rais wa Tanzania, John Magufuli ametuma ujumbe wa rambirambi kwa familia za watu 32 ikiwa ni pamoja na wanafunzi, walimu wawili na dereva wa basi ambao wamekufa katika ajali ya basi la shule Jumamosi asubuhi.

    Wanafunzi hao wa shule ya msingi Lucky Vincent walikuwa wakisafiri kwa basi la shule kutoka shuleni kwao kwenda shule nyingine kwa ajili ya kufanya mitihani.

    Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Bi Theresia Mahongo amesema basi hilo lilitumbukia katika korongo la mto Marera kilomita 150 toka mjini Arusha baada ya kushuka toka kwenye muinuko wa kilima kutokana na utelezi uliosababishwa na mvua.

    Wakati huo huo Rais Magufuli amesema serikali yake ipo tayari kufanya kazi na sekta binafsi ili kuinua uchumi na kuondoa hisia kwamba serikali yake ilikuwa inapambana na biashara, amesema kuwa serikali yake haiwezi kuvumilia ukwepaji wa kodi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

    Magufuli pia ameitaka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) pamoja na taasisi nyingine za serikali kuanza kutoa huduma masaa 24 kila siku kuanzia jumatatu ili kuimarisha biashara nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako