• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ajali ya barabarani yasababisha vifo vya watu wasiopungua 26 nchini Nigeria

    (GMT+08:00) 2017-05-07 17:26:24

    Mabasi mawili jana yaligongana kwenye barabara kuu kati ya miji ya Lagos na Ibadan iliyo kusini magharibi mwa Nigeria, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 26.

    Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani jimboni Oyo Bw. Yusuf Salami amesema mabasi hayo yalishika moto mara moja baada ya kugongana.

    Kwa upande wake, msemaji wa polisi wa jimbo hilo Bw. Adekunle Ajisebutu amesema watu 26 walikufa kwa kuteketea kwa moto na wengine 11 wakiwemo watoto wamejeruhiwa na sasa wanatibiwa katika hospitali.

    Mashuhuda wa ajali hiyo walisema miili ya abiria waliofariki iliungua vibaya kiasi cha kushindwa kutambulika

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako