• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makamu wa Rais wa Tanzania kuongoza waombolezaji kutoa heshima za mwisho kwa wahanga wa ajali ya basi ya Arusha

    (GMT+08:00) 2017-05-08 09:13:59

    Makamu wa Rais wa Tanzania Bibi Samia Suluhu Hassan leo anatazamiwa kuongoza waombolezaji kutoa heshima za mwisho kwa watoto wa shule waliofariki kwenye ajali ya basi iliyotokea mapema Jumamosi.

    Shughuli ya kutoa heshima ya mwisho itafanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha. Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, makamu wa rais ataambatana na mawaziri, maofisa wa ngazi ya juu wa serikali pamoja na wabunge. Awali Bw Gambo alisema shughuli hiyo ilipangwa kufanyika Jumapili, lakini iliahirishwa hadi Jumatatu ili kutoa nafasi ya watu zaidi kushiriki.

    Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya shule Bw Severine Lasway, amesema idadi ya vifo imefika 36, wakiwemo wanafunzi 33, walimu wawili na dereva. Ripoti za awali zilionesha kulikuwa na watu 35 kwenye basi hilo, lakini baada ya miili kutolewa kwenye basi imeonekana kuwa kulikuwa na watu zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako