• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yapandisha mara mbili gharama kibali cha kuwatazama mlima sokwe walio hatarini kutoweka

    (GMT+08:00) 2017-05-08 18:36:38

    Bodi ya Maendeleo ya Rwanda RDB imesema nchi hiyo imeongeza gharama za kibali cha watalii wote wanaotaka kuwatazama mlima sokwe kutoka dola za kimarekani 750 hadi dola za kimarekani 1500.

    Kifurushi kipya kwa watalii ambao wanaotaka kutazama familia nzima ya sokwe pia kinauzwa kwa dola za kimarekani 15,000 na kutoa huduma bora zaidi na binafsi za uongozaji wa utalii. Ongezeko hilo la bei litakaloanza mara moja halitawaathiri watalii walikwisha kata tiketi zao kabla ya mabadiliko hayo mapya.

    Ongezeko hilo linalenga kuongeza juhudi za uhifadhi na kuchangia zaidi maendeleo ya jamii zinazoishi katika maeneo yaliyo karibu na Hifadhi ya Taifa ya Volkano, wanakoishi sokwe hao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako