• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji 34 wa kundi la IS wauawa mashariki mwa Afghanistan

    (GMT+08:00) 2017-05-08 18:38:57

    Kituo cha propaganda cha kundi la IS kimeharibiwa huku wapiganaji 34 wa kundi hilo wakiuawa baada ya jeshi la Afghanistan kushambulia maficho ya kundi hilo katika mkoa wa Nangarhar ulioko mashariki mwa nchi hiyo.

    Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya ndani ya Afghanistan imesema, mashambulizi hayo yalifanywa na jeshi la ulinzi la Afghanistan siku moja iliyopita katika wilaya za Achin na Naziyan, na kwamba jeshi hilo litaendelea kulenga maeneo ya magaidi hao katika sehemu nyingine nchini humo.

    Vikosi vya Marekani nchini Afghanistan leo vimethibitisha kuwa kiongozi wa juu wa kundi la IS nchini humo, Sheikh Abdul Hasib aliuawa katika operesheni ya pamoja iliyofanyika mkoa wa Nangarhar mwishoni mwa mwezi uliopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako