• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watalii waliotembelea Tanzania yaongezeka kwa asilimia 12.9 kwa mwaka jana

    (GMT+08:00) 2017-05-09 10:35:42

    Naibu waziri wa maliasili na utalii wa Tanzania Bw. Ramo Makani amesema, idadi ya watalii wanaoingia Tanzania imeongezeka kwa asilimia 12.9 mwaka jana.

    Bw. Makani alisema hayo wakati akijibu swali la mbunge kuhusu jinsi nchi hiyo itakavyoshughulikia ongezeko la idadi ya watalii nchini humo. Amesema, serikali inafanya juhudi kuboresha miundombinu, viwanja vya ndege na aina mbalimbali za bidhaa za kitalii.

    Bw. Makani ameongeza kuwa wamechukua hatua kuboresha sekta ya utalii, pia wametambua baadhi ya vivutio vipya vya utalii ambavyo viko katika mpango wa maendeleo wa miaka mitano kutoka 2016/17 hadi 2020/21.

    Kwa mujibu wa naibu waziri huyo, idadi ya watalii waliotembelea Tanzania kwa mwaka 2016 ilikuwa 1,284,279, ikilinganishwa na 1,137,182 ya mwaka juzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako