• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Kenya yawasaka wauaji wa faru katika hifadhi ya wanyama

    (GMT+08:00) 2017-05-09 10:36:29

    Mamlaka ya wanyamapori Kenya KWS inawasaka majangili waliomwua faru jike na kukata pembe zake katika hifadhi binafsi ya wanyamapori iliyoko katikati nchini humo.

    Msemaji wa KWS Bw. Paul Gathitu amesema, walinzi wa hifadhi hiyo wamemwokoa mtoto wa faru ambaye aligunduliwa karibu na mwili wa mama yake katika hifadhi ya Solia.

    Bw. Gathitu pia amesema, operesheni inayofanywa imegundua nyayo zinazoshukiwa kuwa za majangili walioingia kwenye hifadhi hiyo binafsi. Kutokana na uungaji mkono kutoka angani, wamegundua mwili wa faru mmoja mdogo anayekadiriwa kuwa na umri wa wiki tatu ambaye alikatwa pembe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako