• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Upanuzi wa kiwanda cha kampuni ya magari ya China BAW nchini Afrika Kusini waanza

  (GMT+08:00) 2017-05-09 16:58:25

  Hafla ya mradi wa upanuzi wa kiwanda cha kampuni ya kutengeneza magari ya Beijing (BAW) nchini Afrika Kusini imefanyika jana mkoani Gauteng, Afrika Kusini.

  Akizungumza kwenye hafla hiyo, mkuu wa tawi la kampuni hiyo nchini Afrika Kusini Bw. Zhang Wei amesema, mradi huo utakaogharimu dola za Marekani milioni 18.36 unalenga kupanua wigo wa utengenezaji wa vipuri vya magari nchini Afrika Kusini, kutoa nafasi zaidi za ajira na kupunguza matumizi ya utengenezaji wa magari.

  Pia amesema, mradi huo utamalizika mwezi Machi mwaka ujao na kutoa nafasi za ajira zaidi ya 100 kwa watu wa nchi hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako