• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mamia ya wahamiaji wahofiwa kufa kwenye ajali mbili za meli katika bahari ya Mediterranean

  (GMT+08:00) 2017-05-09 16:59:33

  Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema, wahamiaji 245 wanahofiwa kufa katika ajali mbili za kuzama kwa boti zilizotokea katika Bahari ya Mediterranean wikiendi iliyopita.

  Kwa mujibu wa msemaji wa UNHCR Cecile Pouilly, ajali ya kwanza ilitokea usiku wa Ijumaa baada ya boti moja iliyokuwa na watu 132 kuzama katika Bahari ya Mediterranean.

  Watu 50 wameokolewa na kupelekwa kwenye kisiwa cha Sicily, Italia, huku wahamiaji wengine 82 waliokuwa kwenye boti hiyo wakielekea nchi za Ulaya wakihofiwa kufa.

  Katika ajali ya pili iliyotokea Jumapili katika pwani ya Syria, watu 163 kati ya watu 170 waliokuwemo kwenye boti iliyozama wanahofiwa kufa maji ama hawajulikani walipo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako