• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashindano ya lugha ya kichina kwa wanafunzi wa shule za sekondari yafanyika nchini Tanzania

    (GMT+08:00) 2017-05-09 17:56:22

    Mashindano ya kwanza ya lugha ya kichina kwa wanafunzi wa shule za sekondari yamefanyika Jumapili mjini Dodoma, Tanzania.

    Washindani 12 kutoka shule 6 wameshiriki katika mashindano hayo ya kusikiliza, kuandika, kuhutubia na kuzungumza lugha ya kichina. Katika mashindano hayo, Saada Jumbo kutoka shule ya sekondari ya Morogogo alibuka mshindi. Saada amesema anapenda sana kujifunza Kichina, na ana matumaini kwamba iko siku atakwenda kusoma nchini China na kuelewa zaidi utamaduni wa China.

    Kwenye mashindano hayo, wanafunzi hao pia wamefanya maonesho ya kungfu kwa watazamaji wapatao 200.

    Tanzania ilianza kufanya majaribio ya kutoa mafunzo ya lugha ya kichina katika shule 6 za sekondari mwaka jana, na kufikia mwishoni mwa mwaka huo, wanafunzi 2,631 walikuwa wamejifunza lugha hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako