• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa msaada wa dharura wa kibinadamu kwa Nigeria

    (GMT+08:00) 2017-05-09 17:56:42

    Serikali ya China imetoa msaada wa dharura wa kibinadamu kwa Nigeria katika hafla iliyofanyika katika ghala la nafaka la Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP lililo karibu na Maiduguri, mji mkuu wa jimbo la Borno nchini humo.

    Katika hafla hiyo, Balozi wa China nchini Nigeria Zhou Pingjian amemkabidhi mkurugenzi wa ofisi ya Shirika hilo nchini Nigeria Bw. Ron Sibanda msaada huo wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 5, ambao utasaidia WFP kununua mchele kwenye masoko ya Nigeria na ya kimataifa ili kuwasaidia Wanigeria milioni 4.1 waliokimbia makazi yao.

    Kutokana na mashambulizi ya kundi lenye siasa kali la Boko Haram, watu wengi wamekimbia makazi yao kaskazini mashariki mwa Nigeria, ambapo takwimu kutoka WFP zinaonesha kuwa, hadi mwezi Machi mwaka huu, idadi ya watu hao imefikia milioni 1.8.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako