• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Sekta ya madini kufufuliwa na wawekezaji

    (GMT+08:00) 2017-05-09 19:06:17

    Baada ya hasara ya miaka miwili kutokana na kuporomoka kwa bei ya kimataifa ya madini,sekta ya madini nchini Rwanda inatarajia kuimarika tena kufuatia wawekezaji wapya kutoka Marekani.

    Peterson Tumwebaz mkurugenzi na muanzilishi wa shirika la ujasiriamali wa madini linalofanya shuhuli zake katika nchi zaidi ya 60 amebashiri mambo makubwa baina ya shirika lake na Rwanda.

    Kupitia kwa mahojiano na vyombo vya habari nchini Rwanda,mkurugenzi huyo amesema Rwanda itafaidika pakubwa na ushirikiano baina ya pande hizo mbili.

    Rwanda ikiwa ni moja ya nchi zilizo na ekolojia (Eco system) bora ni kituo muafaka cha kuvumbua madini ya thamani.

    Wawekezaji wameanza kuvutiwa na Rwanda kutokana na kuwpo kwa jukwaa bora lisilo na vikwazo vingi vya biashara.

    Aidha kasi ya ukuwaji wa uchumi wa Rwanda imetajwa kuwa kichocheo kingine cha uwekezaji.

    Shirika hilo la Marekani limewekeza dola milioni 13 za mtaji pekee katika sekta ya madini na dola milioni 18 za harakati .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako