• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Kenya kufaidika na bilioni 53.4 za Uingereza

    (GMT+08:00) 2017-05-09 19:07:10

    Kenya ni miongoni mwa nchi zitakazofaidika na fedha za uwekezaji za Uingereza za takriban bilioni 53.4.

    Fedha hizi za shirika la ndege la British Airways Kevin Leunge anasema fedha hizo zitatumika katika kuboresha vituo vya uwanja wa ndege wa jomo Kenyatta ili kuimarisha huduma za abiria.

    Mbali na hayo wakaazi wa Nairobi nchini Kenya watalazimika kuendelea kutumia fedha zaidi za kununua maji ya matumizi yao ya biashara na nyumbani.

    Hii ni baada ya kampuni ya usambazaji maji nchini Kenya kutangaza kwamba uhaba wa maji uliopo jijini Nairobi na viunga vyake utaendelea kutokana na ukosefu wa maji.

    Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo,ijapokuwa mvua inaonyesha kwa wingi usambaji wa maji wa kawaida hautaraejea kawaida hadi pale viwango vya maji kwenye bwawa la ndakaini kufikia asilimia 30.

    Mbaruku Vyakweli afisa mkuu wa masuala ya kampuni hiyo amesema hadi sasa viwango vya maji Nairobi viko chini ya asilimia 25 hivyo wakaazi wataendelea kupata maji kwa mgao na kununua.

    Mtungi mmoja wa maji unauzwa shilingi 40.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako