• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Mvua yasababisha hasara kubwa Katavi

    (GMT+08:00) 2017-05-09 19:07:26

    Wafanyibiashara wa mkoa wa Katavi Tanzania wamepata hasara ya mamilioni ya fedha baada ya mvua kubwa kuharibu mali yao .

    Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Raphael Muhuga, amesema hasara halisi iliyosababishwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha katika kijiji cha Kasansa kilichopo katika wilaya ya Mlele imefikia zaidi ya Sh milioni 780.

    Kikosi cha wataalamu kimetahmini jumla ya hasara ya yaliyosababishwa na mvua iliyosababisha mafuruko makubwa katika kijji cha Kasansa kwamba hasara halisi ni Sh 709,780,041.

    Akifafanua alisema tathmini inaonesha kuwa hasara halisi ya uharibifu wa miundombinu ikiwemo ya miradi ya umwagiliaji na barabara iliyosababishwa na mvua hiyo ni Sh 591,228,041, thamani ya uharibifu wa mazao ni Sh 89,562,041 na vifaa na mali vya thamani ya Sh 28,9990,000 viliharibiwa.

    Waliofariki walitambuliwa kuwa ni pamoja na ndugu watatu wa familia moja, Isabela Milambo (14 ) aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la sita, Jane Milambo (10) ambaye alikuwa mwanafunzi wa darasa la nne na Mwasi Milambo (5) ambaye alikuwa hasomi. Wengine ni Revinus Joseph (10), mwanafunzi wa darasa la nne na Anjela Justin, aliyekuwa na umri wa wiki, Leduisi Suwi (6) mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Kilida iliyopo katika kata ya Kasansa ambaye mzazi wake aitwae Moses Suwi anafundisha katika shule hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako