Rais Xi Jinping wa China amempigia simu rais mteule wa Ufaransa Emmanuel Macron.
Rais Xi amempongeza Macron kwa kuchaguliwa kuwa rais wa Ufaransa, na kusisitiza kuwa China inatilia mkazo uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na inapenda kuungana mkono na Ufaransa katika masuala makubwa, na kuimarisha ushirikiano wa kihalisi katika pande mbalimbali. Amesema China inaikaribisha Ufaransa kushiriki kwenye ujenzi wa Ukanda Mmoja na Njia Moja.
Rais mteule Macron amesema serikali mpya ya Ufaransa itashikilia dira ya kirafiki kuhusu China, kushikilia sera ya kuwepo kwa China moja, na kuimarisha ushirikiano wa kihalisi katika mambo ya diplomasia, uchumi, biashara, viwanda na ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja".
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |