• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw Moon Jae-in achaguliwa kuwa rais wa Korea Kusini

    (GMT+08:00) 2017-05-10 09:57:21

    Takwimu zilizotolewa na tume ya uchaguzi ya Korea Kusini zinaonyesha kwamba Bw Moon Jae-in kutoka Chama cha Kidemokrasia amechaguliwa kuwa rais mpya wa Korea Kusini.

    Kati ya asilimia 88.7 ya kura zilizohesabiwa Bw Moon Jae-in amepata asilimia 40.3 na kufanyikiwa kumshinda mpinzani wake Bw Hong Joon-pyo na kuthibitishwa kuwa rais mpya wa Korea Kusini. Wagombea wengine Bw Ahn Cheol-soo na Bw Hong Joon-pyo wamekubali kushindwa.

    Habari zinasema Bw Moon Jae-in ataanza kazi mara moja baada ya kupata uthibitisho kutoka kwa tume ya uchaguzi.

    Ikulu ya Marekani imempongeza Bw Moon Jae-in kwa ushindi wake na kusema itashirikiana na Korea Kusini chini ya uongozi wa Bw Moon Jae-in.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako