• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pendekezo la Ukanda moja na Njia moja ni mchango muhimu kwa kutatua masuala ya dunia

    (GMT+08:00) 2017-05-10 10:24:40

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. António Guterres, amesema pendekezo la Ukanda moja na Njia moja la China ni mchango muhimu katika kutatua masuala yanayoikabili dunia nzima ikiwemo suala la mabadiliko ya hali ya hewa.

    Bw. Guterres ambaye atafanya ziara nchini China wiki hii na kuhudhuria Mkutano wa Baraza la Ukanda moja na Njia moja, amesema pendekezo la China linaendana na ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa, na anatarajia kuwa baraza hilo litahimiza ajenda hiyo, na kuzisaidia nchi zinazoendelea kukabiliana na changamoto zilizopo.

    Pia amesistiza umuhimu kwa nchi mbalimbali kuunganisha utekelezaji wa pendekezo la Ukanda moja na Njia moja na ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 na mikakati yao ya maendeleo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako