• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais mpya wa Korea Kusini ateua waziri mkuu na mkuu wa shirika la ujasusi

  (GMT+08:00) 2017-05-10 16:22:32

  Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini amemteua waziri mkuu mpya, mkuu wa shirika la ujasusi, mnadhimu mkuu wa ikulu, na mkuu wa huduma ya usalama wa rais.

  Lee Nak-yon, mkuu wa mkoa wa Jeolla Kusini, ametajwa kuwa waziri mkuu katika serikali ya rais Moon. Uteuzi wake utawasilishwa katika bunge la nchi hiyo, na ataanza kutekeleza majukumu yake baada ya kupitishwa na bunge hilo.

  Rais Moon pia amemteua Im Jong-seok kuwa mnadhimu mkuu wa ikulu, huku Suh Hoon akiteuliwa kuchukua wadhifa wa mkuu wa shirika la ujasusi la Korea Kusini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako