• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatoa mwito wa kuharakisha mchakato wa kupunguza umaskini duniani

  (GMT+08:00) 2017-05-10 16:33:10

  Balozi wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Liu Jieyi ametoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kuharakisha mchakato wa kupunguza umaskini, na kusukuma mbele mawasiliano na ushirikiano wa kimataifa wa aina mpya wa kupunguza umaskini ili kupata mafanikio kwa pamoja.

  Bw. Liu amesema hayo kwenye mjadala wa kawaida wa baraza la jamii na uchumi la Umoja wa Mataifa. Amesema pande mbalimbali zinatakiwa kuboresha uhusiano wa wenzi wa maendeleo duniani, na kuendeleza ushirikiano wa nchi zaKaskazini-Kusini na nchi za Kusini-Kusini. Amesema Umoja wa Mataifa na Benki ya Dunia zinatakiwa kuendelea kutoa mchango mkubwa, na nchi zilizoendelea zinatakiwa kutimiza ahadi za kuzisaidia nchi zinazoendelea kuinua uwezo, kupunguza au kufuta madeni, kufungua masoko, na kuzisaidia kutatua matatizo ya kujiendeleza.

  Ameongeza kuwa China imewasaidia jumla ya watu maskini milioni 700 waishio vijinini nchini humo kuondokana na umaskini nchini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako