• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rooney asema atasalia kwenye klabu yake Manchester United

    (GMT+08:00) 2017-05-12 08:48:50

    Mchezaji wa klabu ya Manchester United, Rooney kwa msimu huu ameweza kucheza michezo 22 pekee katika michezo yote ndani ya kikosi chake, huku wakala wake akionekana kuja hapa China mwanzoni mwa Mwaka huu akijaribu kuzungumza na vilabu vinavyovutiwia na huduma ya mchezaji huyo. Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Uingereza ambaye ni mfungaji wa Muda wote, amesema anahitaji kusalia ndani ya kikosi cha Manchester United lakini hakuelezea atasalia katika kikosi hicho cha Mashetani wekundu mpaka lini.

    Akizungumza katika Mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo wao wa nusu fainali wa Europa League dhidi ya klabu ya Celta Vigo, Rooney amekiri kuwepo na maelewano mabovu kati yake na kocha wake Jose Mourinho. Na alipoulizwa kuhusu maisha yake ya baadae na United amesema amekuwa katika klabu hiyo kwa takribani miaka 13, hivyo bila shaka anahitaji kucheza mpira.

    Rooney pia aliongeza kusema kuwa lengo lake lilikuwa ni kuisaidia United kuingia fainali za Europa League huko Stockholm, jambo ambalo litawapa nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako