• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yaihimiza Afrika kuimarisha kampuni za bima ili kustawisha biashara

    (GMT+08:00) 2017-05-12 09:58:12

    Rais Uhuru Kenyatta amezihimiza serikali za nchi za Afrika kuimarisha mashirika ya bima ili kusaidia kuunga mkono biashara ndani ya bara hilo.

    Kwenye hotuba yake iliyosomwa na waziri wa fedha Bw. Henry Rotich kwenye mkutano mkuu wa 17 wa Bima ya Biashara ya Afrika ATI, rais Kenyatta pia amezitaka serikali za nchi za Afrika kufikiria uanachama wa ATI.

    Rais Kenyatta amesema, nchi za Afrika zimesaini Makubaliano ya Biashara Huria ya Bara hilo, kwa lengo la kuhimiza ukuaji wa biashara kati ya nchi za Afrika, pamoja na kuzisaidia nchi za bara hilo kunufaika na biashara ikiwa nguvu ya ukuaji na maendeleo endelevu.

    ATI inafanya kazi ya kuhimiza biashara za ndani na nje ya bara hilo kupitia mfumo wake wa kupunguza hatari, na kuwapatia uhakikisho wawekezaji wa ndani na nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako