• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali mpya Sudan yatangazwa

    (GMT+08:00) 2017-05-12 10:10:38

    Waziri mkuu wa Sudan Bw Hassan Saleh ametangaza kuundwa kwa serikali mpya ya Sudan.

    Bw Saleh amesema luteni jenerali Mohamed Othman Rukabi ameteuliwa kuwa waziri wa fedha, Bw Mubarak Fadel al-Mahdi ameteuliwa kuwa waziri wa uwekezaji, Bw Abdulrahman Othman Abdulrahman atakuwa waziri wa mafuta, na Bw Hamed al-Mannan atakuwa waziri wa mambo ya ndani.

    Chama tawala cha Sunda NCP kimepewa nafasi za wizara za ulinzi, mambo ya nje, mafuta, fedha, elimu na elektroniki.

    Serikali mpya ilitarajiwa kutangazwa mwezi Februari mwaka jana, lakini uamuzi huo uliahirishwa kutokana na maoni tofauti kati ya vyama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako