Rais Xi Jinping wa China amekutana na waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn aliyeko hapa Beijing kuhudhuria kongamano la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" litakaloanza Jumapili wiki hii.
Kwenye mazungumzo hayo, rais Xi amependekeza kuinua uhusiano kati ya nchi hizo kuwa uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote. Pia amesema China itaiunga mkono Ethiopia kutumia pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" kuonesha nafasi yake ya kama daraja na kiunganishi katika ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika.
Kwa upande wake, waziri mkuu Hailemariam amesema Ethiopia na China zimepata maendeleo makubwa katika ushirikiano wao kwenye sekta za uchumi, biashara, uwekezaji, viwanda na miundo mbinu. Amesema Ethiopia itajitahidi kushiriki kwenye ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja", kwani pendekezo hilo lina maana kwa dunia nzima, na litahimiza mawasiliano na ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |