• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanasayansi wathibitisha aina mpya ya dinosaur na kuipa jina la "dinosaur mchanga kutoka China"

    (GMT+08:00) 2017-05-12 19:09:17

    Utafiti mpya ulitolewa kwenye gazeti la Nature Communications unasema baada ya kutafiti mabaki ya yai lenye kiinitete cha dinosauri yaitwaye "Baby Louie", wanasayansi wamegundua dinosaur mkubwa wa aina mpya ya jenasi ya Oviraptor, na kuipa jina la "Beibeilong Sinensis" ambalo lina maana ya dinosaur mchanga kutoka China.

    Dinosaur wa aina hiyo wenye urefu wa mita 8 na uzito wa tani 3 waliishi katika miaka milioni 80 iliyopita, na ni aina ya pili iliyogunduliwa ya dinosaur wa jenasi ya Oviraptor. Mwanapaleontolojia wa Canada Dr. Darla Zelenitsky alisema huenda dinosaur wa Beibeilong alifanana na ndege mkubwa asiyeweza kuruka.

    Mwishoni mwa miaka ya 80 na mwanzoni mwa miaka ya 90 karne iliyopita, wakulima waligundua maelfu ya mayai ya dinosaur mkoani Henan, China, ambalo moja lenye urefu wa milimita 45 ndilo la "Baby Louie". Baadaye yai hilo liliuzwa kwa njia haramu na kufika Marekani. Yai hilo liliwahi kuoneshwa katika jumba la makumbusho la watoto la Indianapolis. Mwaka 2013, na lilirudishwa nchini China, kuhifadhiwa katika jumba la makumbusho la jiolojia la mkoa wa Henan, na wanasayansi walianza kulitafiti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako