Rais Xi Jinping wa China leo asubuhi kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la "Ukanda Mmoja na Njia moja", ametoa hotuba kuhusu "Kushirikiana katika kusukuma mbele ujenzi wa Ukanda mmoja na Njia moja". Amesema, njia ya Hariri ya kale yenye umbali wa malefu ya kilomita na historia zaidi ya miaka elfu moja, imelimbikiza moyo wa njia ya Hariri unaozingatia ushirikiano na amani, uwazi na ushirikiano, kufundishana na kunufaishana, ambao ni urithi muhimu wa Ustaarabu wa binadamu. Tangu enzi za Tang, Song na Yuan kwenye historia ya China, njia za Hariri ziliendelea ardhini na baharini, ambapo wasafiri mashuhuri wa China, Italia na Morocco ambao ni Du Huan, Macro Polo na Ibn Battuta wote waliwahi kuacha nyayo zao kwenye njia hizo. Shughuli hizo hazikufanyika kwa farasi wa kivita na mkuki, bali kwa msafara wa ngaramia na nia njema, na hazikutegemea manowari na mizinga, bali ni meli za kibiashara na urafiki.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |