• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Xi Jinping: Ukuaji wa uchumi duniani unahitaji msukumo mpya

    (GMT+08:00) 2017-05-14 09:32:18

    Rais Xi Jinping wa China amesema, kwa mtizamo wa historia, jamii ya binadamu iko kwenye enzi ya maendeleo makubwa, mageuzi makubwa na marekebisho makubwa. Kwa mtizamo wa hali halisi, dunia yetu inakabiliwa na changamoto nyingi zinazoibuka mara kwa mara. Ukuaji wa uchumi wa dunia unahitaji msukumo mpya, tunahitaji maendeleo yenye uwiano zaidi yanayowanufaisha watu wengi zaidi, na pengo kati ya maskini na mataraji linapaswa kupunguzwa. Migogoro ya kikanda inaendelea kupamba moto huku ugaidi ukiendelea kuenea na kusababisha majanga. Nakisi katika masuala ya amani, maendeleo na usimamizi imekuwa changamoto kubwa inayokabili binadamu wote. Katika miaka minne tangu Pendekezo la Ukanda mmoja na Njia moja litolewe, nchi na mashirika ya kimataifa zaidi ya 100 kote duniani yameunga mkono na kushiriki kwenye pendekezo hilo, na Baraza kuu la Umoja wa Mataifa na Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa pia limejumuisha pendekezo hilo, ambalo limeanza kutekelezwa hatua kwa hatua na kupata mafanikio mengi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako