Benki ya uwekezaji wa miundombinu ya Asia AIIB imetoa mkopo wa dola bilioni 1.7 za kimarekani kwa miradi 9 ya nchi washirika wa Ukanda Mmoja na Njia moja, na uwekezaji wa Mfuko wa Njia ya Hariri umefikia dola bilioni 4 za kimarekani. Hayo yamesemwa na rais Xi Jinping wa China kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la "Ukanda Mmmoja na Njia moja". Rais Xi amesema China ikishirikiana na nchi washirika wa Ukanda mmoja na Njia moja, zinaendelea na juhudi za kurahisisha biashara na uwekezaji na kuboresha mazingira ya kibiashara, na juhudi hizo zimeonesha ufanisi. Kuanzia mwaka 2014 hadi mwaka 2016, thamani ya biashara kati ya China na nchi washirika wa Ukanda mmoja na Njia moja ilizidi dola trilioni 3 za kimarekani, na katika kipindi hicho, China iliwekeza zaidi ya dola bilioni 50 katika nchi za Ukanda mmoja na Njia moja.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |