• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuimraisha uungaji mkono wa kifedha kwa ujenzi wa Ukanda Mmoja na Njia Moja

    (GMT+08:00) 2017-05-14 09:53:03

    Rais Xi Jinping wa China amesema, katika juhudi za kuimarisha uungaji mkono wa kifedha kwa ujenzi wa Ukanda mmoja na Njia moja, China itatoa nyongeza ya yuan bilioni 100, sawa na dola bilioni 14.5 za kimarekani, kwenye mfuko wa Njia ya Hariri. Amesema, Benki ya maendeleo ya China CDB na benki ya exim ya China zitatoa mikopo maalum ya yuan bilioni 250 na bilioni 130 mtawalia, kwa ajili ya kuunga mkono ujenzi wa miundombinu na ushirikiano wa kiviwanda na kifedha katika Ukanda mmoja na Njia moja. Mbali na hayo, China pia itajitahidi kuendeleza ushirikiano wa kibiashara wa kunufaishana na nchi washirika wa Ukanda mmoja na Njia moja. Katika kipindi cha Baraza la Mkutano wa Ukanda mmoja na Njia moja, China itasaini mikataba ya ushirikiano wa kiuchumi na nchi zaidi ya 30, na kujadiliana na nchi husika kuhusu Makubaliano ya Biashara huria FTA. Rais Xi pia amesema China itaandaa Maonesho ya kimataifa ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje CIE kuanzia mwaka kesho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako