• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kuagiza bidhaa dola trilioni 8 kutoka nje katika miaka mitano ijayo

  (GMT+08:00) 2017-05-14 11:21:30

  Akihutubia Mkutano wa Baraza la Ukanda mmoja na Njia moja, naibu waziri mkuu wa China Bw. Zhang Gaoli amesema, katika miaka mitano ijayo, China itaagiza bidhaa zenye thamani ya dola trilioni 8 za kimarekani kutoka nje, kuvutia uwekezaji wa kigeni dola bilioni 600, huku ikiwekeza dola bilioni 750 kwa nje. Aidha, katika kipindi hicho, idadi ya watalii wa China wanaotembelea nchi za nje inatarajiwa kufikia milioni 700. Bw. Zhang Gaoli amesema, China inazikaribisha nchi mbalimbali duniani kutumia kwa pamoja fursa zinazotokana na maendeleo yake, na kusisitiza kwamba mambo ya ujenzi wa "Ukanda mmoja na Njia moja" yatajadiliwa kwa pamoja, kutekelezwa kwa pamoja na kunufaika kwa pamoja na nchi zote washirika. Bw. Zhang anatumai kuwa wajumbe wanaohudhuria mkutano huo watachangia busara na nguvu zao katika kusukuma mbele Ujenzi wa "Ukanda mmoja na Njia moja" na kujenga Jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako