• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kilele wa Baraza la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" wafanyika hapa Beijing

    (GMT+08:00) 2017-05-14 18:29:18

    Mkutano wa kilele wa Baraza la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" umefanyika hapa Beijing, rais Xi Jinping wa China amehudhuria ufunguzi wa mkutano huo na kutoa hotuba kuhusu "Kushirikiana katika kusukuma mbele ujenzi wa Ukanda Mmoja na Njia Moja".

    Kwenye hotuba yake, rais Xi amesema, Kwa mtizamo wa hali halisi, dunia yetu inakabiliwa na changamoto nyingi zinazoibuka mara kwa mara. Ukuaji wa uchumi wa dunia unahitaji msukumo mpya, tunahitaji maendeleo yenye uwiano zaidi yanayowanufaisha watu wengi zaidi, na pengo kati ya maskini na mataraji linapaswa kupunguzwa. Migogoro ya kikanda inaendelea kupamba moto huku ugaidi ukiendelea kuenea na kusababisha majanga. Nakisi katika masuala ya amani, maendeleo na usimamizi imekuwa changamoto kubwa inayokabili binadamu wote. Katika miaka minne tangu Pendekezo la Ukanda mmoja na Njia moja litolewe, nchi na mashirika ya kimataifa zaidi ya 100 kote duniani yameunga mkono na kushiriki kwenye pendekezo hilo, na Baraza kuu la Umoja wa Mataifa na Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa pia limejumuisha pendekezo hilo, ambalo limeanza kutekelezwa hatua kwa hatua na kupata mafanikio mengi.

    Rais Vladimir Putin wa Russia pia ameonesha matarajiao mema kuhusu mustakabali wa "Ukanda Mmoja na Nji Moja", huku akisema kuwa mpango huo umeleta fursa kwa ushirikiano wa siku za mbele kati ya bara al Ulaya na la Asia, wanapongeza sana na kuunga mkono mpango huo, rais Xi amewaoneshea nguvu ya mfano wa kuigwa. Wana imani kuwa kupitia utaribu wa muungano wa uchumi wa Ulaya na Asia, "Ukanda Mmoja na Njia Moja" na Shirika la Ushirikiano la Shanghai, maendeleo ya utandawazi wa Ulaya na Asia yatasukumwa mbele.

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres aliyehudhuria mkutano huo amesema, mpango wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" unatokana na historia, China imekuwa nguvu kuu ya dunia yenye pande mbalimbali. Katika ajeda ya 2030 na makubaliano ya Paris, China imetoa mchangu muhimu sana. China pia imetoa mfululizo wa maazimio ikiwemo Benki ya AIIB. Na maazimio hayo yenyewe ni muhimu sana, kwa sababu dunia yenye ncha mbalimbali inahitaji utatuzi wa pande mbalimbali.

    Imefahamika kwamba mkutano huo umewashirikisha wajumbe 1500 hivi kutoka nchi zaidi ya 130 na mashirika zaidi ya 70 ya kimataifa, wakiwemo viongozi 29 wa nchi za nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako