• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Simba Sports Club yapata udhamini wa Sportpesa, Hans Poppe abwaga manyanga

    (GMT+08:00) 2017-05-15 08:32:39
    Klabu maarufu ya kandanda nchini Tanzania, Simba, imepata udhamini wa miaka mitano kutoka kwa kampuni ya SportPesa ambayo wiki hii imezindua rasmi uchezaji wa kamari kwa kubashiri matokeo ya kandanda nchini humo.

    Mkurugenzi wa usimamizi wa SportPesa nchini Tanzania Abbas Tarimba amesema timu zingine zitafaidika kwani kampuni hiyo inataka kubadilisha kabisa sura ya michezo nchini Tanzania.

    Wakati hayo yakijiri, Mjumbe wa kuteuliwa wa Kamati ya Utendaji, Zacharia Hans Poppe ameuandikia uongozi wa klabu hiyo barua ya kujiuzulu, akilalamikia kutoshirikishwa katika mkataba wa SportPesa.

    Hans Poppe aliyekuwa pia Mwenyekiti wa Kamati za Usajili na mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Bunju Complex, amezungumza na baadhi ya waandishi wa habari za michezo jijini Dar es salaam na kuthibitisha kujiuzuru kwake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako