Mkutano wa tano wa washauri bingwa duniani umefanyika hapa Beijing, na kuhudhuriwa na wataalamu na wasomi zaidi ya mia moja kutoka ndani na nje ya China, ambao walijadiliana kwa kina kuhusu ajenda ya maendeleo endelevu duniani.
Kwenye ufunguzi wa mkutano huo, naibu mwenyekiti wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China Bw. Chen Yuan amesema, anataka mkutano huo uwashirikishe na kuwashawishi washauri, wataalamu na wasomi wa sekta mbalimbali kutumia vizuri mwelekeo wa maendeleo ya utandawazi, kuhimiza mageuzi ya usimamizi wa dunia na kanuni za kimataifa, na kushiriki kwenye mpango wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja". Pia kutafiti na kukabiliana na changamoto mbalimbali duniani, kutoa mpango na ufumbuzi ulio wazi na wenye ufanisi na kusukuma mbele uundaji wa njia mpya ya maendeleo ya dunia yenye haki, ujumuishi, maslahi ya pamoja na endelevu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |