• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Yemen yatangaza hali ya hatari ya afya huko Sanaa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu

    (GMT+08:00) 2017-05-15 18:48:49

    Wizara ya afya ya umma na idadi ya watu ya Yemen inetangaza hali ya hatari ya afya huko Sanaa kutokana na kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu, ambao umesababisha vifo vya watu 115 toka Aprili, 27.

    Shirika la habari la Saba la Yemen limeinukuu wizara ya afya nchini humo ikisema kuwa tangazo la hali ya hatari lilitolewa baada ya ugonjwa huo kuenea kwenye wilaya za mji wa Sanaa, na maeneo ya pembezoni ya mji huo.

    Idadi ya watu walioambukizwa ugonjwa huo imefikia 2,567 katika wiki mbili zilizopita, ambayo imezidi kiasi cha kawaida, na mfumo wa afya nchini Yemen hauwezi kukabiliana na maafa hiyo isiyotarajiwa ya kiafya .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako