Rais Xi Jinping wa China leo amesema Ukanda Mmoja na Njia Moja ni pendekezo lililotolewa na China, lakini unamilikiwa na dunia nzima, na kwamba mlango wake uko wazi kwa marafiti wote wenye nia moja, na hauzuii wala kulenga upande wowote.
Rais Xi amesema hayo kwenye mazungumzo ya kilele wa meza ya duara yaliyofanyika wakati wa Kongamano la Kilele la Ushirikiano wa Kimataifa la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" linalofanyika hapa Beijing.
Rais Xi pia amesema, kiini cha pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" ni kuhimiza ujenzi wa miundombinu na maingiliano, kuunganisha sera na mikakati ya maendeleo ya nchi mbalimbali, kuimarisha ushirikiano wa kivitendo, na kuhimiza maendeleo ya pamoja, ili kutimiza ustawi wa pamoja.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |