• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Unga kushuka baada ya wiki mbili...waziri

    (GMT+08:00) 2017-05-15 19:22:59

    Bei ya unga wa mahindi itaanza kupungua katika muda wa wiki mbili zijazo, waziri wa kilimo Willy Bett alisema jana.

    Bw Bett alisema kwamba alikutana na wakuu wa viwanda vya kusaga nafaka Alhamisi iliyopita na wakaafikiana kushusha bei ya unga mara baada ya kupokea mahindi yaliyoingizwa humu nchini kutoka mataifa ya kigeni.

    Serikali imetoa mwanya wa miezi miwili unusu wafanyibiashara kuingiza mahindi humu nchini bila kutozwa ushuru.

    Bw Bett anasema kuwa magunia elfu 335,000 ya mahindi kutoka Mexico yatari yamefika katika bandari ya Mombasa.

    Aidha amesema itachukua muda wa siku tatu kupakua mahindi kutoka kwenye meli hiyo na kisha kusafirishwa hadi katika viwanda vya kusaga nafaka.

    Kamishana wa Udhibiti wa Mipaka wa KRA Julius Musyoka amesema mahindi meupe yataingizwa humu nchini bila ushuru hadi julai tarehe 31 huku yale ya manjano yakiruhusiwa hadi Agosti 31.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako