• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirikisho la mchezo wa Hockey: Strathmore yaibuka washindi

    (GMT+08:00) 2017-05-16 08:35:41
    Timu ya hockey ya wanawake ya chuo Kikuu cha Strathmore, imesalia katika nafasi ya tatu kwenye msururu wa ligi ya shirikisho la mchezo huo nchini Kenya. Hii ni baada ya kuishinda timu ya Chuo Kikuu cha Kenyatta mabao 3-0 kwenye uwanja wa City Park jijini Nairobi.

    Katika mechi nyingine za wanawake zilizochezwa mwishoni mwa juma, Chase Amira iliicharaza timu ya Chuo Kikuu cha Nairobi mabao 6-0. Katika mechi za ligi za wanaume, timu ya Chuo Kikuu cha Kenyatta iliipiku timu ya chuo cha ufundi bao 1-0 huku Butali Sugar Warriors ikinyakua ushindi wa 2-1 dhidi ya Wazalendo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako