• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ujerumani na Ufaransa kutunga mpango wa maendeleo wa muda wa kati na mrefu wa Umoja wa Ulaya

  (GMT+08:00) 2017-05-16 15:17:39

  Ujerumani na Ufaransa zitapanga mpango wa maendeleo wa muda wa kati na mrefu wa Umoja wa Ulaya, na zinapenda kuvunja mikataba inayotekelezwa ya Umoja huo kwa ajili ya kuufanyia mageuzi.

  Makubaliano haya yalifikiwa jana kati ya Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na rais Emmanuel Macron wa Ufaransa mjini Berlin. Bi. Merkel amesema huu ni wakati muhimu kwa maendeleo ya Umoja wa Ulaya, na anapenda kufanya ushirikiano wa kuaminiana na kirafiki na rais Macron. Pia amesema mbali na kushughulikia suala la Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya, mpango wa maeneleo pia utaangalia kuimarisha Umoja huo, haswa maendeleo ya eneo linalotumia Euro na kuongeza uwezo wa kukabiliana na hali ya dharura ya Umoja wa Ulaya.

  Kwa upande wake, rais Macron amesema eneo linalotumia Euro linahitaji uwekezaji mpya ili kufufua uchumi, lakini haikubaliki kushirikisha nchi za eneo hilo kutoa dhamana ya pamoja kuzisaidia nchi nyingine za eneo hilo zenye tatizo la kiuchumi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako