• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa walaani Korea Kaskazini kurusha makombora

    (GMT+08:00) 2017-05-16 18:26:15

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na Baraza la Usalama la Umoja huo kwa pamoja wameilaani Korea Kaskazini kwa kurusha tena makombora, na kuihimiza kufuata njia ya kuondoa silaha za nyuklia.

    Taarifa iliyotolewa na msemaji wa katibu mkuu huyo imesema, Bw. Guterres amesema kitendo hicho kimevunja azimio la Baraza la Usalama na kutishia usalama wa kikanda. Ametoa wito kwa nchi hiyo kuahidi kufuata majukumu ya kimataifa na kuondoa silaha za nyuklia.

    Nalo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesema linafuatilia kitendo hicho cha Korea Kaskazini. na kusema litatekeleza kikamilifu azimio la Baraza hilo dhidi ya Korea Kaskazini na kama ikihitajika, linawezekana kuweka vikwazo zaidi dhidi ya nchi hiyo.

    Habari zinasema, Korea Kaskazini imefanya majaribio ya makombora tarehe 29 mwezi uliopita na Jumapili iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako