• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Mauzo ya chai Uingereza yashuka baada ya nchi hiyo kujitoa umoja wa ulaya

    (GMT+08:00) 2017-05-16 19:32:24

    Kenya hivi sasa inashuhudia athari za Uingereza kujitoa kwenye nchi zinazotumia sarafu ya Euro kufuatia kupungua kwa kiwango cha chai kinachonunuliwa na Uingereza wakati nchi za ulaya zikiamua kuipa kisogo Uingereza na kuagiza bidhaa hiyo moja kwa moja.

    Ripoti ya utendaji wa sekta ya chai iliyotolewa na Mkurugenzi wa chai inaonyesha kuwa kiwango kilichonunuliwa na Uingereza kilipungua kutoka kilo 5.4milioni mwezi Machi mwaka jana hadi kilo 3.1milioni kipindi kama hicho mwaka huu.

    Kurugenzi ya chai inaonyesha kuwa Uingereza hainunui tena chai kwa kiwango kikubwa kutoka Kenya kutokana na kupungua kwa soko la uuzaji katika nchi nyingine za ulaya ambazo zimekuwa zikinunua bidhaa hiyo kutoka Uingereza.

    Mkuu wa kurugenzi ya chai Samuel Ogola amesema kupungua huko kumesababishwa na Brexit,kwani Uingereza ilikuwa mnunuzi mkubwa wa chai ya Kenya ambayo ilikuwa ikinunua kwa matumizi ya nyumbani na pia kuuza kwa nchi nyengine za ulaya.

    Wataalam mwaka jana walionya kuwa kujiondoa kwa Uingereza kutoka kwa Umoja wa Ulaya kutasababisha kushuka kwa kiwango cha chai ambacho Uingereza inaagiza kutoka Kenya kutokana na kushuka kwa masoko yake ambayo huuza chai hiyo.

    Uingereza ni muuzaji mkubwa wa chai ya Kenya.Mwkaa 2014 iliuza asilimia 17 ya bidhaa hiyo iliyoagiza kutoka Kenya kwa mataifa ya Ireland,Ujerumani,Poland na Ufaransa ambayo ndio masoko yake makubwa.

    Ogola amesema nchi ambazo zilikuwa zikinunua chai ya Kenya kutoka Uingereza hivi sasa zinanunua moja kwa moja kutoka Kenya.

    Ripoti hiyo inaonyesha kuwa kiwango cha chai kilichosafirishwa Poland na Ujerumani kimeongezeka kwa asilimia 39 na 12 mtawalia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako