• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mikopo sekta binafsi yapungua Tanzania

    (GMT+08:00) 2017-05-16 19:34:11

    Licha ya Serikali nchini Tanzania kuongeza Shilingi bilioni 880.9 kwenye mzunguko wa fedha, taasisi za biashara zimepunguza mikopo kwenda sekta binafsi, taarifa ya Benki Kuu (BoT) inaonyesha.

    Ripoti ya kila mwezi ya BoT iliyotolewa Aprili, inaonyesha ujazo mpana wa fedha (M3) umekua kwa asilimia 4.1 hadi kufikia Sh22.54 trilioni mpaka mwishoni mwa Machi. Hata hivyo, kiasi hicho ni kidogo ikilinganishwa na mwaka ulioishia Machi mwaka jana kulipokuwa na ongezeko la asilimia 15.5.

    Kupungua huko, ripoti imesema, kumechangiwa na woga wa benki za biashara kuikopesha sekta binafsi na kuongezeka kwa ukopaji wa Serikali kutoka kwenye taasisi hizo za fedha.

    Mikopo iliyotolewa kwa sekta binafsi ilikuwa Sh603 bilioni ikilinganishwa na Sh855 iliyoelekezwa serikalini. Mikopo ya sekta binafsi, imepungua kwa takriban asilimia 20 ikilinganishwa na ilivyokuwa Machi mwaka jana kiasi hicho kilipoongezeka kwa asilimia 23.6.

    Sekta ya usafirishaji na mawasiliano imeathirika zaidi baada ya mikopo yake kupunguzwa kwa asilimia 21.6 mwezi huo ikiwa ni baada ya kupungua kwa asilimia 2.6 Februari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako