• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya China inajenga kituo cha teknolojia za ujenzi Kenya

    (GMT+08:00) 2017-05-17 09:21:35

    Kampuni ya Wu Yi ya China inaharakisha ujenzi wa kituo cha teknolojia za ujenzi mjini Nairobi, na mpaka sasa imewekeza zaidi ya dola milioni 100 za kimarekani kwenye ujenzi wa kituo cha utafiti, mistari ya uzalishaji na duka la vifaa vya ujenzi, vitakavyoanza kufanya kazi baadaye mwaka huu.

    Naibu mkuu wa Kampuni ya Wu Yi nchini Kenya Bw Lin Yihua amesema baada ya kukamilika, kituo hicho kitakuwa ni jengo la kisasa lenye mkusanyiko wa vitu mbalimbali vinavyohusiana na uzalishaji, utafiti, mauzo na maonesho ya vifaa vya ujenzi.

    Kampuni ya Wu Yi ilianza kazi nchini Kenya mwaka jana kwa lengo la kuboresha sekta ya ujenzi wa nyumba nchini humo na kwenye eneo kubwa zaidi la mashariki kwa Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako