• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yataka hatua kuchukuliwa kuzuia vifo vya vijana wa Afrika

    (GMT+08:00) 2017-05-17 09:49:23

    Shirika la Afya Duniani WHO limesema Serikali za Afrika na wadau wao wa maendeleo wanapaswa kuwekeza mipango ya kupunguza kiwango cha vifo vya vijana vinavyotokana na magonjwa yanayozuilika.

    Katika ripoti yake iliyotolewa mjini Nairobi, shirika hilo limesema nchi za Afrika kusini mwa Sahara zinachukua asilimia 45 ya vifo vya vijana takriban milioni 1.2 vinavyotokea kila mwaka duniani.

    Akizungumzia hali ya vifo hivyo Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa WHO Flavian Bustreo amesema idadi ya vifo vya vijana ni wito kwa wadau kuongeza uwekezaji katika huduma za kinga na tiba kwa vijana, ambao wamekuwa wakisahaulika kwenye mipango ya afya ya taifa.

    Ripoti hii mpya inapendekeza kuwepo kwa mikakati kama kutoa elimu ya kina ya jinsia mashuleni, kuweka ukomo wa umri kwa wanywaji pombe, kupunguza uchafuzi wa ndani na kutekeleza sheria ya kupambana na matumizi mabaya ya silaha za moto ili kuzuia vifo vya vijana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako