• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 4 wauawa katika mlipuko Dadaab, Kenya

    (GMT+08:00) 2017-05-17 09:56:44

    Watu wanne waliuawa jana baada ya gari walilokuwa wakisafiria kukanyaga bomu la kutengenezwa kienyeji katika eneo la Dadaab, Kaskazini Mashariki mwa Kenya.

    Ofisa wa serikali ya huko Bw. Mohamud Saleh amesema, huenda bomu hilo lilitegwa na wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab wakati wa usiku. Amesema serikali inaamini kuwa waliokuwa wanalengwa ni maofisa wa usalama wanaofanya doria kwenye mpaka wa Garissa, lakini ni bahati mbaya lililipua gari binafsi.

    Tangu Kenya ilipotuma jeshi lake nchini Somalia kupambana na kundi la Al-Shabaab, maofisa wa Kenya wanaofanya doria kwenye mpaka na Somalia wanashambuliwa mara kwa mara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako