• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lajadili suala la majaribio ya makombora yaliyofanywa na Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2017-05-17 19:57:23

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana limejadili kitendo cha Korea Kaskazini kufanya majaribio ya makombora, na kulaani vikali kitendo hicho.

    Mwenyekiti wa zamu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambaye pia ni balozi wa Uruguay kwenye Umoja huo Bw. Elibio Rosselli amesema, ameisisitiza Korea Kaskazini isifanye uchunguzi wa nyuklia na majaribio ya makombora. Pia amesema nchi wajumbe wa Baraza hilo walijadili hatua za kukabiliana na hali ya sasa, zikiwemo vikwazo na diplomasia ya amani.

    Bw. Roselli amesema Baraza la Usalama limesisitiza kuwa ni muhimu sana kwa Korea Kaskazini kuonesha ahadi yake ya kutotumia silaha za nyuklia kwa vitendo halisi, na kufanya juhudi kutuliza mvutano kwenyePeninsula ya Korea na sehemu nyingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako