• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa kilele wa Baraza la kimataifa la "Ukanda mmoja, Njia moja" ni hatua za utekelezaji wa majukumu za China

  (GMT+08:00) 2017-05-17 20:05:19

  Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Hua Chunying amesema, Mkutano wa kilele wa Baraza la kimataifa la "Ukanda mmoja, Njia moja" umetoa fursa muhimu kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, kutimiza maendeleo ya pamoja na kuonesha utekelezaji wa majukumu wa China ikiwa nchi kubwa duniani.

  Akizungumzia baadhi ya nchi zinazodai kuwa lengo la China kuandaa mkutano huo ni kuongeza ushawishi na uongozi wake duniani,

  Bi Hua Chunying amesema, pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja lililotolewa na China linafuata kanuni ya kujadiliana, kujenga kwa pamoja na kunufaishwa kwa pamoja. Amesema China inashikilia kanuni ya kuzitendea nchi zote bila ya kujali ni nchi kubwa au ndogo, lakini pia inaona kuwa nchi kubwa yenye maliasili nyingi na uwezo mkubwa zaidi zinapaswa kubeba majukumu makubwa zaidi na kuchangia kiasi kikubwa zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako