• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF yasema Tanzania inaweza kuwa nchi yenye mapato ya kati kwa kufanya uchumi kuwa shirikishi

    (GMT+08:00) 2017-05-18 09:16:25

    Shirika la fedha la kimataifa IMF limesema Tanzania inaweza kufikia hadhi ya kuwa nchi yenye mapato ya kati kama itafanya ongezeko la uchumi wake liwe shirikishi zaidi.

    Akiongea mjini Dar es salaam naibu mkurugenzi wa IMF Bw Tao Zhang amesema, sekta binafsi inatakiwa kuwa na nafasi muhimu katika kuhimiza maendeleo ya uchumi, pamoja na kuwekeza zaidi kwenye sekta ya nishati ili kuvutia wawekezaji zaidi.

    Bw Tao pia amesema serikali ya Tanzania inatakiwa kufanya mchakato wa kufanya maamuzi uwe wazi na wa kutabirika, kwenye kanuni na taratibu zake. Pia amehimiza mafungamano zaidi kwenye jumuiya ya Afrika Mashariki ili kupanua zaidi biashara na uwekezaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako