• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ronaldo kuwa kivutio kikuu kwenye fainali ya Klabu Bingwa Ulaya

    (GMT+08:00) 2017-05-18 09:38:26

    Huku fainali ya dimba la Klabu Bingwa Ulaya ikiwa imeratibiwa kutandazwa Juni 3, 2017 katika uwanja wa Cardiff kati ya Real Madrid na Juventus, wadadisi sasa wanaonya kuwa Christiano Ronaldo wa Real ndiye atakuwa kivutio kikuu. Huku kukiwa hakuna shaka kuwa Klabu hizi mbili zina uthabiti wa kipekee katika fomu zao, Real ikiwa ndiyo bingwa mtetezi wa kombe hilo inatathminiwa kuwa na msukumo wa kipekee wa kuibuka na ushindi.

    Juve ilitwaa kombe hilo mara ya mwisho miaka 21 iliyopita huku Real ikiwa imelinyanyua kombe hilo mara 11. Kocha wa Real Zinedine Zidane, amesema, hawawazii kuhusu kushinda au kushindwa, ila kuingia dimbani na kutekeleza haki kwao na mashabiki wao.

    Old Lady, kama wanavyojiita Juventus kwa upande wao wanafahamika kwa ugumu wa ngome yake mbele ya lango lao.

    Ilitinga fainali baada ya kuwazamisha miamba wa Uhispania FC Barcelona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako